top of page
aronsanga2

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 10.12.2023



Kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Kalvin Phillips, 28, yuko kileleni mwa orodha ya wanunuzi wa Manchester United msimu ujao wa joto. (Sun)

Manchester United inamfuatilia mshambuliaji wa RB Leipzig na Ubelgiji Lois Openda, 23, wakati wakitafuta kuchukua nafasi ya winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, na mhambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 28, msimu ujao. (Mirror)

Newcastle wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Crystal Palace wa Uingereza Sam Johnstone, 30. (Star)


Manchester City wanavutiwa na mlinzi wa Club Brugge Tajon Buchanan mwezi Januari na watalazimika kulipa takribani pauni milioni 50 kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Canada mwenye umri wa miaka 24. (Star)


Newcastle United wanapanga kufanya usajili wa mkopo kutoka Saudi Pro League mwezi Januari. (Football Insider)

Wolves wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 7 mwezi Januari kwa kiungo wa kati wa Burnley Muingereza Josh Brownhill, 27. (Mirror).


Rais wa Barcelona Joan Laporta anapanga kufanya mazungumzo kuhusu mustakabali wa wachezaji wawili wa Ureno Joao Felix, 24, kwa mkopo kutoka Atletico Madrid, na Joao Cancelo, 29, kwa mkopo kutoka Manchester City. (Sport - in Spanish)

Manchester United wainaongoza Tottenham katika kinyang'anyiro cha kumsajili mlinzi wa Nice wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 23. (Football Insider)

Everton wamekataa ofa kutoka Tottenham ili kubadilisha masharti ya mkataba wa pauni milioni 10 uliokubaliwa kama sehemu ya uhamisho wa kiungo wa kati wa zamani wa Uingereza Dele Alli, 27, kwenda Goodison Park Januari 2022. (Times).


Mshambuliaji wa Reading mwenye umri wa miaka 18, Caylan Vickers yuko tayari kuhamia kwa miamba ya Uhispania Real Madrid. (Sun)

Manchester United imeulizia kuhusu mshambuliaji wa Guinea na Stuttgart Serhou Guirassy, ​​27, ambaye anaweza kupatikana kwa chini ya euro 20m (£17m). (Sky Sports Ujerumani)

Bayern Munich wamemfanya mchezaji wa Barcelona Ronald Araujo, 24, kuwa mlengwa wao mkuu wa uhamisho na wanaweza kulipa ada "kubwa" kwa mlinzi huyo wa Uruguay. (Sky Sports Ujerumani).


Mshambuliaji wa zamani wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic, ambaye alistaafu mwishoni mwa msimu uliopita, anasema "anazungumza" na AC Milan kuhusu kurejea katika klabu hiyo katika baadhi ya nafasi. (Sky Sports Italia)

Juventus wanafuatilia hali ya kiungo mshambuliaji wa Brazil Felipe Anderson, 30, ambaye kandarasi yake huko Lazio inakamilika msimu wa joto. (Calciomercato)

1 view0 comments

Comments


bottom of page